Chebukati ndiye shujaa wa uchaguzi huu-Ruto ampongeza mwenyekiti wa IEBC

"Ninataka kumshukuru mshindani wangu anayestahili kwa kampeni ambayo sote tulizingatia maswala na kujaribu kuuza ajenda

Muhtasari
  • Naibu rais aliwashukuru Wakenya kwa kuwa na subira akisema uchaguzi ulithibitisha kuwa Wakenya walikuwa wamepanda ngazi ya kisiasa zaidi ya ukabila
Naibu rais William Ruto na waumini baada ya ibada Karen
Naibu rais William Ruto na waumini baada ya ibada Karen
Image: Facebook//WILLIAM RUTO

Naibu rais na rais mteule wa uchaguzi mkuu wa 2022 William Ruto amemsherehekea Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Wafula Chebukati akimtaja kama shujaa baada ya kutangazwa kuwa rais mteule.

Katika hotuba yake ya ushindi, Ruto alisema IEBC ilionyesha uwazi katika kazi yake akisema kila mtu yuko katika nafasi ya kupata matokeo na kuwa na hesabu zake. Aidha alisema anashukuru kwa kushinda vikwazo vyote na kupata kura.

"Shujaa wa uchaguzi huu ni IEBC ambao wametushangaza na matokeo kwenye tovuti na ulichohitaji ni kikokotoo kupata matokeo. Nataka kusema bila woga wa kupingana kuwa Wafula Chebukati ndiye shujaa wetu.

Ninataka kumshukuru Mungu kwamba tuko hapa kushuhudia wakati watu wa Kenya wakirejesha kwamba mamlaka yote ni ya watu wa Kenya. Ninajua kulikuwa na ubashiri kwamba singeweza kupiga kura," Ruto alisema.

Naibu rais aliwashukuru Wakenya kwa kuwa na subira akisema uchaguzi ulithibitisha kuwa Wakenya walikuwa wamepanda ngazi ya kisiasa zaidi ya ukabila.

Ruto alithamini juhudi ambazo mpinzani wake mkuu Raila Odinga alikuwa ameweka akisema angekuwa kiongozi jumuishi katika utawala wake na kuongeza kuwa angejenga kutoka ambapo rais Uhuru Kenyatta ameondoka.

"Ninataka kumshukuru mshindani wangu anayestahili kwa kampeni ambayo sote tulizingatia maswala na kujaribu kuuza ajenda, nitashirikiana na viongozi wote waliochaguliwa na viongozi wote nchini Kenya ili tusimuache mtu yeyote nyuma.