Ruto ang'aa nyumbani kwa Mudavadi

Ruto alipata kura 22,087 huku Raila akiwa na kura 19,743.

Muhtasari

•Sabatia ni nyumbani kwa kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi, ambaye alimtema Raila Odinga na kujiunga na Ruto kwenye Kenya Kwanza.

DP Ruto awasili Bomas katika uzinduzi wa azma ya urais wa Mudavadi
Image: Ezekiel Aming'a

Mgombea urais wa UDA William Ruto alipata kura nyingi zaidi katika eneo bunge la Sabatia, kaunti ya Vihiga.

Sabatia ni nyumbani kwa kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi, ambaye alimtema Raila Odinga na kujiunga na Ruto kwenye Kenya Kwanza.

Ruto alipata kura 22,087 huku Raila akiwa na kura 19,743.

Wagombea urais George Wajackoyah wa chama cha Roots na David Mwaure w a Agano walipata kura 330 na 126 mtawalia.

Idadi ya waliojiandikisha kupiga kura katika eneo bunge hilo ilikuwa 70,875.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema kura 42,286 kati ya zilizopigwa zilikuwa halali.

Idadi ya kura zilizokataliwa ilikuwa 343.