Waandamanaji wawasha moto katika barabara ya Mwingi kufuatia matokeo ya kura

Waandamanaji walliimba haki yetu, haki yetu ya kura.

Muhtasari

•Wafuasi wa Muema Nduku aliyepoteza kiti cha MCA wa wadi ya Kyuso waliandamana na kuwasha moto katika barabara ya Kyuso-Mwingi.

Afisa wa polisi akisafisha barabara ya Kyuso-Mwingi iliyofungwa kwenye daraja la Kamuwongo kaunti ya Kitui Jumatatu.
Afisa wa polisi akisafisha barabara ya Kyuso-Mwingi iliyofungwa kwenye daraja la Kamuwongo kaunti ya Kitui Jumatatu.
Image: MUSEMBI NZENGU

Machafuko yalikumba soko la Kamuwongo eneo bunge la Mwingi Kaskazini kaunti ya Kitui Jumatatu huku wafuasi wa timu pinzani wakizozana.

Wafuasi wa Muema Nduku aliyepoteza kiti cha MCA wa wadi ya Kyuso waliandamana na kuwasha moto katika barabara ya Kyuso-Mwingi.

Wakazi hao waliokuwa na ghadhabu wakiongozwa na aliyeshindwa katika uchaguzi huo, waliwasha moto na kufanya magari kutoweza kupita.

Waliimba haki yetu, haki yetu ya kura.

Waandamanaji wawasha moto katika barabara ya Mwingi kufuatia matokeo ya kura
Waandamanaji wawasha moto katika barabara ya Mwingi kufuatia matokeo ya kura
Image: MUSEMBI NZENGU

Wakazi hao waliokasirika, wengi wao wakiwa wanawake, walibeba mabango yenye jumbe za kumsifu Muema huku wengine wakidai Haki.

Walidai kuwa mgombea wao alitapeliwa na kumpendelea John Munyoki Mwinzi wa Wiper ambaye alitangazwa mshindi.

Muema na wafuasi wake walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari karibu na magurudumu yenye moto kwenye daraja la Kamuwongo, gari la polisi aina ya land cruiser lilifika likiwa na maafisa wa polisi waliokuwa na silaha ambao waliwataka waandamanaji hao kutawanyika bila mafanikio.

Maafisa hao wa usalama kisha walilazimika kuwarushia vitoa machozi waandamanaji ambao walitawanyika kabla ya kujipanga tena huku wakicheza na kuimba nyimbo za kumsifu Muema.Lakini Muema ambaye wakati fulani alibebwa bega juu alifanikiwa kuwashawishi wafuasi wake kuondoka eneo la tukio.