Kila upande kuwa na mawakili wasiopungua 4 katika Mahakama ya Juu - Amadi

Maamuzi ya maombi yote ya kujiunga yatawasilishwa mtandaoni kabla ya saa tano asubuhi Jumanne.

Muhtasari
  • "Sio kila mtu ataruhusiwa kuingia. Vyama vina timu kubwa lakini idadi italazimika kuzuiwa kwa sababu nafasi haiwezi kuchukua kila mtu," alisema.
Msajili Mkuu wa Mahakama Ann Amadi
Image: DOUGLAS OKIDDY

Msajili Mkuu wa Mahakama Ann Amadi anasema ni mawakili wanne pekee kutoka kwa kila upande ndio watakaoruhusiwa kufikia chumba cha mahakama.

"Sio kila mtu ataruhusiwa kuingia. Vyama vina timu kubwa lakini idadi italazimika kuzuiwa kwa sababu nafasi haiwezi kuchukua kila mtu," alisema.

"Tunajua watu wengi watataka kushiriki kwa kuingia lakini hili halitawezekana kwa sababu tunaruhusu vyombo vya habari kutangaza kwa umma....Hatutaki kuingia kwenye matatizo na usimamizi wa umati."

Majaji wote saba watakuwepo kwenye kesi inatarajiwa kuanza saa tano asubuhi Jumanne.

Maamuzi ya maombi yote ya kujiunga yatawasilishwa mtandaoni kabla ya saa tano asubuhi Jumanne.