Labda mpango wa Uhuru ulikuwa kukabidhi mamlaka kwa Ruto - Mutahi Ngunyi

Matamshi hayo yanajiri baada ya Mahakama ya upeo kutangaza kwa kauli moja uchaguzi wa Ruto kuwa halali.

Muhtasari
  • Mahakama ilitoa uamuzi huo siku ya Jumatatu baada ya kusikizwa kwa kesi hizo kukamilika siku ya Ijumaa

Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Mutahi Ngunyi amedai kuwa rais Uhuru Kenyatta a, muda wote huo, alikuwaamepanga kukabidhi mamlaka kwa rais mteule William Ruto.

Katika taarifa baada ya uamuzi wa Mahakama ya Juu kuunga mkono ushindi wa Ruto, Ngunyi alionekana kupendekeza kuwa Rais Uhuru hakufanya vya kutosha kuhakikisha kinara wa Azimio La Umoja Raila Odinga anashinda kiti cha urais.

"Labda Raila alikuwa tapeli na mpango wa Uhuru wakati wote ulikuwa wa kumkabidhi Ruto. Nasema hivyo kwa sababu Uhuru alitenda kwa njia ndogo katika uchaguzi huu. Alimkabidhi Ruto eneo bunge lake bila vita. Kisha akalemaza jimbo la kina. huu ni mpango wa Kumi-Kumi?" Ngunyi alisema.

Matamshi hayo yanajiri baada ya Mahakama ya upeo kutangaza kwa kauli moja uchaguzi wa Ruto kuwa halali.

Raila na wengine sita walikuwa wamehamia katika Mahakama ya upeo ya Kenya kupinga kutangazwa kwa Ruto kama Rais na Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati.

Mahakama ilitoa uamuzi huo siku ya Jumatatu baada ya kusikizwa kwa kesi hizo kukamilika siku ya Ijumaa.

Mahakama ilisema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kwamba naibu rais anayeondoka alipata 50 pamoja na moja zinazohitajika ili mmoja atangazwe rais.