Mahakama kutoa uamuzi wa kesi ya uchaguzi wa urais kuanzia saa sita mchana

Mahakama ilitangaza hayo Jumatatu katika notisi iliyotumwa kwa vyombo vya habari.

Muhtasari

•Jaji Mkuu Martha Koome mnamo Ijumaa alisitisha rasmi kusikilizwa kwa kesi ya rais kabla ya hukumu ya leo.

•Majaji walitumia wikendi nzima kuandika uamuzi wao kuhusu masuala tisa yaliyowasilishwa mahakamani siku tatu zilizopita katika ombi la kupinga kuchaguliwa kwa Naibu Rais William Ruto kuwa Rais Mteule.

Benchi la majaji saba likiongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome, naibu CJ Lady Justice Philomena Mwilu, Jaji Mohammed Ibrahim, Jaji Dkt. Smokin Wanjala, Lady Justice Njoki Ndungu, Jaji Isaac Lenaola na Jaji William Ouko wakati wa kongamano la kesi kabla ya kuanza kwa ombi la urais katika Mahakama ya Juu Agosti 30, 2022.
Image: DOUGLAS OKIDDY

Mahakama ya Upeo itatoa maamuzi yake Jumatatu kuhusu kesi ya rais mwendo wa sa sita, Mahakama imesema. 

Mahakama ilitangaza hayo Jumatatu katika notisi iliyotumwa kwa vyombo vya habari.

Benchi la majaji saba linatarajiwa kutoa hukumu zao wenyewe na kuzisoma katika Mahakama ya Upeo.

Saba hao ni pamoja na; Jaji Mkuu Martha Koome, Philomena Mwilu (Naibu Jaji Mkuu) Njoki Ndung'u, Issac Lenaola, Smokin Wanjala, Mohammed Ibrahim na William Ouko.

Koome mnamo Ijumaa alisitisha rasmi kusikilizwa kwa ombi la rais kabla ya hukumu ya leo. 

Majaji walitumia wikendi nzima kuandika uamuzi wao kuhusu masuala tisa yaliyowasilishwa mahakamani siku tatu zilizopita katika ombi la kupinga kuchaguliwa kwa Naibu Rais William Ruto kuwa Rais Mteule.

 Masuala hayo yaliunda sehemu kubwa ya hoja za mawakili kadhaa waliowakilisha Raila Odinga, Ruto, tume ya IEBC, mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati na wahusika wengine katika kesi hiyo.

Mawakili walikuwa na siku tatu za kutoa hoja na ushahidi mbele ya mahakama ya majaji saba kuanzia Jumatano.  

Kesi hiyo ilianza Jumanne kwa kongamano la kabla ya kesi baada ya walalamishi na walalamikiwa kumaliza kuwasilisha hati zao za kiapo kufikia Jumatatu. 

Mnamo Ijumaa majaji hao waliwaomba Wakenya kuwaombea wawe na utambuzi wanapoandika hukumu hiyo. 

Mwaka wa 2017 mahakama hiyo iliweka historia kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kubatilisha uchaguzi wa rais.