Chege Njuguna atangazwa mgombea wa UDA katika uchaguzi mdogo wa Kandara

Kiti cha Ubunge kiliachwa wazi baada ya Alice Wahome kuteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Usafi wa Mazingira na Rais William Ruto.

Muhtasari
  • Njuguna alitangazwa mshindi katika kura za mchujo za UDA zilizoendeshwa katika eneo bunge hilo Jumamosi baada ya kupata kura 7,826
CHEGE NJUGUNA

Chege Njuguna ametangazwa kuwa mwaniaji wa ubunge kwa tiketi ya chama cha United Democratic Alliance (UDA) katika kinyang'anyiro cha Ubunge wa Kandara.

Njuguna alitangazwa mshindi katika kura za mchujo za UDA zilizoendeshwa katika eneo bunge hilo Jumamosi baada ya kupata kura 7,826.

Mgombea huyo atakabiliana na wagombea kutoka vyama vingine vya siasa wakati wa uchaguzi mdogo mnamo Januari 5, 2023.

Kiti cha Ubunge kiliachwa wazi baada ya Alice Wahome kuteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Usafi wa Mazingira na Rais William Ruto.