MOJA KWA MOJA: Tazama mdahalo wa naibu rais hapa

Mjadala kati ya Gachagua na Karua utafanyika kati ya mbili na saa nne usiku.

Muhtasari

•Wagombea urais wanne na wagombea wenza wao wameidhinishwa kugombea katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Sekretarieti ya Mdahalo wa Rais imepanga Mdahalo wa Naibu Rais katika Chuo Kikuu cha Katoliki  cha Afrika Mashariki (CUEA) huko Karen, Nairobi.

Mdahalo huo utang'oa nanga saa kumi na moja jioni  na utashirikisha wagombea  wenza wanne wa urais kutoka vyama vya Roots, Agano Party, UDA na Azimio la Umoja.

Wagombea urais wanne na wagombea wenza wao wameidhinishwa kugombea katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Mdahalo huo utafanyika katika  awamu mbili.

Awamu ya kwanza kitahusisha wagombea wenza wa wagombea urais ambao umaarufu wao katika kura  tatu za maoni za mwisho ulisimama chini ya 5%.

Wagombea wenza hawa ni Justina Wamae wa Roots Party na Ruth Mucheru wa Agano Party.

Uchambuzi wa kabla ya mdahalo utaanza saa kumi na moja jioni huku mjadala ukianza kupeperushwa  kati ya saa kumi na mbili hadi saa moja unusu jioni.

Zubeida Koome na Francis Gachuri watasimamia mjadala wa kwanza.

Mjadala wa pili utaanza saa mbili usiku hadi saa nne usiku.

Utakuwa kati ya wagombea wenza wa wagombea urais ambao umaarufu wao katika kura tatu za mwisho za maoni ulifikia zaidi ya asilimia 5.

Hawa ni Martha Karua wa Muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya na Rigathi Gachagua wa , UDA.

Mjadala huo utasimamiwa na Sophia Wanuna wa NTV na James Smart wa KTN.