(+Picha) Wakazi wa Kondele waanza sherehe kabla ya matokeo rasmi kutangazwa

"Tunataka kumwambia Chebukati kuwa tumekuwa na subira," alisema Omondi Okello,

Muhtasari

•Wenyeji walibainisha kuwa wamesubiri kwa muda mrefu na ni wakati ambao hatimaye matakwa yao yatatimizwa.

Wakazi wa Kondele washerehekea kabla ya matangazo rasmi ya IEBC.
Wakazi wa Kondele washerehekea kabla ya matangazo rasmi ya IEBC.
Image: FAITH MATETE

Wakaazi wa Kondele mjini Kisumu tayari wanasherehekea huku nchi ikisubiri mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kutangaza matokeo ya urais.

Wenyeji waliozungumza na The Star walibainisha kuwa wamesubiri kwa muda mrefu na ni wakati ambao hatimaye matakwa yao yatatimizwa.

"Tunataka kumwambia Chebukati kuwa tumekuwa na subira," alisema Omondi Okello, mkazi.

Mkazi mwingine Mark Owino alisema, "Tunataka jambo hili lifikie mwisho ili tuweze kuendelea na biashara yetu."

Aliongeza kuwa pia wataendelea kuwa na amani bila kujali matokeo ya uchaguzi wa urais.

"Lakini inapaswa kujulikana kuwa tuna matumaini makubwa kwamba matokeo yanatupendelea."