PATANISHO: Huyu Msichana Amefanya Kijana Wangu Awe Mweusi Kama Makaa!

patanisho.fresh
patanisho.fresh
Sarah alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mama mkwe (Mama Maina) ambaye walikosana mwaka wa 2016, mwezi wa nane.

"Nilioleka na kijana wake mwezi wa January mwaka wa 2016 na nilikuwa naishi Nakuru huku kijana wake akiwa anaishi Eldoret. Sasa bwanangu akanieleza kuwa nafaa kuelekea Eldoret kuishi naye kwani hata nilikuwa mja mzito. Mama mkwe naye hakufurahishwa na hayo kwani hakutaka niishi kule."

"Basi nilipokaribia kujifungua mama mkwe akanieleza nifunganye virago nirudi kwetu. Nikamueleza kuwa singerudi kwani mtoto ni wa kijana wake na tulikuwa tumeelewana tutaishi pamoja," alieleza Sarah.

"Nilipojifungua tukaelekea kwa mama mkwe ili akampatie jina. Hapo tulipofika mle hamna yeyote aliyetaka kuzungumza nasi wala kutizama mtoto. Walitupakulia chakula mida ya saa tano na hapo nikakataa. Asubuhi yake niliondoka huku nikimuacha kijana wake nyumbani," Aliongeza huku akifichua kuwa akiwa na mimba ya miezi minne bwanake alikuwa amemshawishi atoe mimba ila naye akakataa.

Basi shida ni kuwa mama mkwe hakutaka niolewa na kijana wake na katika majibizano yale, mama mkwe alikiri kuwa nilimtusi lakini sikumtusi. Shida ni kuwa bwanangu ananipenda lakini familia yake ndio inapinga ndoa yetu.

Alipopigiwa simu mama Maina, alikatiza mawasiliano yetu pindi tu aliposkia sauti ya Sarah, kabla ya kujibu simu kwa mara ya pili.

"Mimi nakuheshimu sana ndio maana nimechukua simu yako. Mimi ni mkristiano na kama mzazi mtoto wako akueleze kuwa unafaa kulala na mtoto wako na mamake akutusi utahisi vipi?" aliuliza mama Maina.

Nilielekea kwa mama Sarah kumueleza awachane na mtoto wangu akanirushia matusi, kurudi kwa Sarah naye akanitusi na ni mtu mgeni sana kwangu ambaye hatujuani, utahisi vipi? Kama singekuwa Mkristiano ningefanya jambo ambalo hujawahi kuona.

Na hapo namweleza huyu mwanadada atoke kwangu na aende kabisa. Amemfanya kijana wangu awe mweusi kama makaa. Mimi simtaki hata kidogo, sina msamaha wake na sitaki chochote kumhusu, ni watu watundu sana," alieleza zaidi.

"Ni sawa nitaondoka kama hivo ndio wanataka lakini mtoto nitawaachia walee," alisema bi Sarah.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be