Covid-19: 884 waambukizwa, 13 waaga dunia

Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Siku ya Jumapili Kenya iliripoti visa vipya 884 vya Coronavirus ikifikisha jumla ya maambukizo kuwa 130,214.

Taarifa ya waziri wa Afya Mutahi Kagwe inasema kesi mpya zimetokana sampuli 5,377 zilizopimwa katika masaa 24 yaliyoisha. 

Kagwe alisema kutokana na kesi hizo mpya, 843 ni Wakenya wakati 41 ni wageni huku 464 wakiwa wa kike na 420 wakiwa wanaume.

Mgonjwa mchanga zaidi ana mwaka mmoja huku mkongwe zaid akiwa na miaka 110.

Idadi ya vipimo vilivyofanywa kufikia sasa ni 1,468,835 tangu kesi ya kwanza iliripotiwa Machi 2020.

Katika habari za huzuni ni kuwa vifo 13 vimeripotiwa. Hii sasa inamaanisha kuwa jumla ya vifo kufikifia sasa ni 2,117.