Orodha ya toboa siri zilizovuma sana mwaka wa 2021

Muhtasari
  • Kweli kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama kwenye kitengo cha Toboa siri, pia wakishindwa kuziweka na kuzificha huwa wanatoboa zote

Kweli kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama kwenye kitengo cha Toboa siri, pia wakishindwa kuziweka na kuzificha huwa wanatoboa zote.

Mengi yamekuwa maajabu ya musa, na vitendo vya kushangaza ambayo wananchi wengi wamekuwa wakifanya.

Katika makala haya, tutazngatia toboa siri kumi ambazo zimekuwa zikivuma, na ambazo zinavuma mitandaoni baada ya wengi kutoboa na kumwaya mtama.

Mnamo Mei mwaka huu, jamaa mmoja alitoboa siri jinsi alivyo mfunga mke wake ili asiolewe baada ya kumuacha.

Huu hapa usimulizi wake;

Katika kipindi cha toboa siri mwanamume mmoja alisimulia jinsi alimfunga mke wake asiolewe wala kuzaa maishani baada ya kuachwa.

"Nilioa mwanamke mmoja akiwa na mtotto baada ya kulea mtoto wake, nilitoka kazi nikapata amebeba kila kitu na amrudia aliyekuwa mpenzi wake na baba wa mtoto wake

Nililipiza kisasi nilienda kwa mganga, nikasema nataka watengane na wasiwahi oanana tena, nilitumia elfu 2,707

Baada ya muda mwanamke huyo alipelekwa nyumbani kwa mwanamume huyo na akaachwa huko nyumbani na mwanamume huyo akabadilisha namba ya simu

Mganga aliniambia tusirudiane na mwanamke huyo, pia nilimfunga asiolewe wala kuzaa tena, mwezi mmoja uliopita alinipigia simu na kuniambia kwamba anataka turudiane lakini mganga alikataa

Sasa nataka kumtobolea siri kwamba siwezi rudiana naye kwa sababu mganga aliniambia tusirudiane na nilimfunga pia," Alisimulia Mwanamume.

Vile vile wanajambo walipigwa na butwaa baada ya jamaa kuda kwamba familia yake inadhani kwamba ameaga dunia ilhali yuko hai.

Aidha jamaa alitoboa siri jinsi aliharibu uzazi wake baada ya kujitahiri, huku akisababisha kutoweza kuzalisha mwanamke.

Hizi hapa baadhi ya orodha ya toboa siri kumi ambazo zimekuwa zikivuma mitandaoni

https://radiojambo.co.ke/vipindi/toboa-siri/2021-08-18-alikuwa-na-nyoka-ambao-walikuwa-wanalalia-noti-za-elfu-moja-jamaa-atoboa-siri/

https://radiojambo.co.ke/vipindi/toboa-siri/2021-08-16-mama-mkongwe-alinitoa-nguoalitaka-tushiriki-tendo-la-ndoa-jamaa-atoboa-siri/

https://radiojambo.co.ke/vipindi/toboa-siri/2021-10-18-nilinyakua-mpenzi-wa-baba-yangunimempachika-mimba-jamaa-amwaya-mtama/

https://radiojambo.co.ke/vipindi/toboa-siri/2021-07-12-niliharibu-uzazi-wangu-baada-ya-kujitahiri-mwanamume-atoboa-siri/

https://radiojambo.co.ke/vipindi/toboa-siri/2021-07-13-niliwadanganya-marafiki-zangu-kuwa-nafanya-kazi-radiojambo-kama-mtangazaji-mbusi-mwanamume-atoboa-siri/

https://radiojambo.co.ke/vipindi/toboa-siri/2021-07-14-taboo-nina-watoto-wawili-na-mama-wa-kambo-jamaa-atoboa-siri/

Je ni toboa siri ipi kati ya hizi na zingine iliyokuacha mdomo wazi, au ambayo inapaswa kurudiwa tene tena?