(+Video) Bintiye Gidi amsherehekea kwa ujumbe wa kusisimua anapoadhimisha siku ya kuzaliwa

"Shukran binti yangu Marie-Rose, nakupenda pia❤," Gidi alimjibu bintiye.

Muhtasari

•Wakenya kutoka kote nchini wameendelea kutuma jumbe za nia njema kwa mwanahabari huyo mahiri anapoongeza mwaka mmoja zaidi.

•Bintiye Gidi alitengeneza video fupi akicheza piano na kumwimbia babake wimbo wa 'Happy Birthday'.

Gidi na bintiye Marie-Rose
Image: INSTAGRAM// GIDI OGIDI

Leo hii, Septemba 5, mtangazaji wa Gidi na Ghost asubuhi kwenye Radio Jambo Joseph Ogidi almaarufu Gidi anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Wakenya kutoka kote nchini wameendelea kutuma jumbe za nia njema kwa mwanahabari huyo mahiri anapoongeza mwaka mmoja zaidi.

Mashabiki wa kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi pia walichukua fursa kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa mtangazaji wao wanayempenda. Wengi wa waliopiga simu studioni Jumatatu asubuhi walikuwa na jumbe za heri njema kwa Gidi.

Mtangazaji mwenza wa Gidi, Jacob 'Ghost' Mulee pia hakuachwa nyuma huku akimuombea baraka tele maishani.

"Happy birthday Boss wangu Gidi Mungu akupe matakwa yako!!" Ghost alimsherehekea Gidi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Bintiye Gidi, Marie-Rose aliwasisimua wanamitandao wengi kwa ujumbe wake mzuri wa siku ya kuzaliwa kwa baba yake.

Malkia huyo mdogo anayeishi Ufaransa alitengeneza video fupi akicheza piano na kumwimbia babake wimbo wa 'Happy Birthday'.

"Happy birthday to you (*3), Happy birthday dear Daddy, Happy Birthday to you.. Happy birthday baba, tunakupenda sana," aliimba Marie-Rose na kumalizia kwa kutuma busu kwa mzazi huyo wake.

"Shukran binti yangu Marie-Rose, nakupenda pia❤," Gidi alimjibu bintiye.

Sote katika Radio Jambo pia tunamtakia mtangazaji huyo tunayemthamini heri njema za siku ya kuzaliwa. Mola akuongezee miaka zadi Gidi!!