Msanii Samidoh ni rafiki yangu wa karibu-Karen Nyamu afichua haya

Muhtasari
  • Mwanasiasa Karen Nyamu alikana madai kwamba ni mpenziye msanii Samidoh
  • Karen alisema kwamba bibi yake Samidoh anajua ukweli kwamba Samidoh ni rafiki yake wa karibu

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye mwanasiasa na wakili Karen Nyamu ambaye miezi mitatu iliopita alijifungua mtoto na madai kuibuka kwamba ni mwanawe msanii Samidoh.

Ni madai ambaye msanii huyo aliyakana, Karen akiwa kwenye mahojiano alikuwa na haya ya kueleza.

"Samidoh ni rafiki yangu wa karibu, kuhusu baba wa mtoto wangu wacha nisijibu kwa maana ni jambo la familia, lakini najivunia kuwa mama wa mtoto wake

 

Mwaka wa 2022 nitakuwa katika kinyang'anyiro cha uaniaji kiti kimoja jijini Nairobi, wakati nilitoa maoni kwenye mitandao ya kijamii na kumjibu shabiki mmoja na kumwambia wanapaswa kutuhurumia sisi bibi wa pili ilikuwa ni utani tu." Alisema Nyamu.

Huku akizungumzia madai kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki huyo alisema,

"Mimi sijali ambacho watu wanasema, na sina wakati wa kujali wanachosema, Samidoh vile ninavyomjua ni kwamba anapenda familia yake,mkewe na hata watoto wake

Bibi yake anajua ukweli kwamba mimi ni rafiki yake Samidoh."

Pia msanii huyo alisema kwamba hapendi mwanamume ambaye anachukulika lakini mwenye anasimamia familia yake kwa pande zote.