Nilisahau kuandika jina langu kwa maana niliambiwa nina kiharusi cha ubongo-Elizabeth Mumbua

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye Elizabth Mumbua ambaye alipitia masaibu akiwa kwenye ndoa yake.

Elizabeth amebaki tu na meno kumi tu lakini sababu ni ipi?

"Baada ya kuolewa nilipitia mateso mingi sana, meno yangu yamekuwa na shida tangu utotoni, kuna wakati nilipooza nilipokuwa najifungua mtoto wangu wa kwanza

 

Nilikaa hospitalini kwa muda wa miezi miwili,baada ya kutoka hospitalini mume wangu aliitwa kazi mbali na nyumbani, alipokuwa anarudi hakuwa anakuja kwangu lakini alikuwa anaenda kwa mama mkwe

Nilikuwa naambiwa niende nikachunge ng'ombe licha yangu kuwa sioni, nilipoaa mtoto wangu nilipoteza nguvu za kuona kwa kweli nilipitia mateso

Kitu ambacho kinaniuma ni kuwa mtoto wangu ambaye alifanya niwe kipofu sijamuona kwa muda wa mika 19, kuna wakati mama yake wa kambo alimchoma nilipoenda nilifukuzwa nikaambiwa hakuna mtoto ambaye ameungua." Alieleza Mumbua.

Mumbua pia alivunjika mguu mwaka wa 2017 baada ya kuanguka kwenye ghorofa.

"Ilikuwa wakati wa uchaguzi wa mwaka wa 2017, wakati uchaguzi mkuu wa rais kutupiliwa mbali, nilikuwa nimeenda kununua mboga

ilipokuwa narudi kwa nyumba nilisikia mlio wa risasi, sijui nilikanyaga wapi nilijipata hospitali, niliambiwa nina 'STROKE BRAIN' au ukipenda kiharusi cha ubongo

Huwa nasahau vitu vingi, nikichukua kalamu niandike jina langu siwezi andika kwa maana nilisahau, nikijaribu kukumbuka naumwa na kichwa

 

Huwa natamani sana kuanza biashara lakini siwezi kwa maana siwezi kumbuka kitu chochote."

Baada ya kutoka katika ndoa yake aliolewa na mwanamume ambaye kwa sasa anamtesa kila wakati huku akimchapa.

Elizabeth alisema kwamba walifungiwa nyumba mwaka jana Novemba, na akaenda kuishi na rafiki yake.

"Kutoka tufungiwe nyumba mume wangu hajawahi nitafuta, ni kama alifurahi sana vile nyumba ilifungwa

Ndugu zangu hawanipendi, nataka tu mtu anisaidie." 

Kwa haya na mengi tembelea Radiojambo youtube.

Pia kama wahitaji kumsaidia Elizabeth unaweza kumfikia kwa hii namba 0728299810.