Watu wengi huniogopa endapo wanataka niwe mpenzi wao-Letoya Johnstone

Muhtasari
  • Johnstone Letoya asimulia maisha yake ya kuwa wanamke lakini ana hisia za mwanamke
Letoya Johnstone
Image: Radiojambo

Leo hii katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye mtetezi wa haki za kibinadamu Letoya Johnstone ambaye alizaliwa akiwa na jinsia ya uume 'Transgender.'

Huku akielezea maisha yake na jinsi alivyogundua kuwa yeye ni mwanamke Transgender alikuwa na haya ya kusema.

"Nilizaliwa nikiwa mwanamume ambapo nilikua nikiwa na hisia za mwanamke, hata nikiwa mchanga nilikuwa na valia mavazi ya mwanamke

 

Mimi ni mwanamke lakini nilizaliwa kwa mwili ambao si wangu yaani mwili wa mwanamume,mimi sijawahi enda kufanyiwa upasuaji kama watu wengine ili kuweka matiti au mambo mengine ya mwanamke

mimi najipenda jinsi nilivyo na ninajikubali licha ya watu wengi kunikejeli, pia sijawahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzii watu wengi huniogopa kama wanataka niwe mpenzi wao

Kuna wakati watu waliniita jini, lakini mimi nimejikubali jinsi nilivyo, wazazi wangu walikuwa wanafikiria tu ni hali ya utoto nilipokuwa mtoto na navaa mavazi ya mwanamke

Mama yangu na baba yangu walikuwa wavuvi." Alizungumza Letoya.

Letoya alisema kwamba watu wa jinsia hiyo hupitia changamoto nyingi kwa maana hawajakubalika katika jamii na hata wengi hawajajikubali.