Nina wake wawili na wote wanajuana na kupendana-Muigizaji Omosh afichua haya

Muhtasari
  • Muigizaji Omosh afichua kuwa ana wake wawili na kuwa wote wanajuana na kupendana
  • Pia alisema kwamba anajuta angekuwa na mtu wa kumshauri wakati alikuwa anabugia vileo, kwa maana hangekuwa mahali alipo sasa
Joseph Kinuthia
Image: Ivy Muthoni

Leo hii katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye muigizaji Joseph Kinuthia almaarufu Omosh, kwa muda Omosh alifahamika kuwa mwenye kupenda kubugia vileo sana.

Lakini sababu ya kubugia vileo ni nini alikuwa na haya ya kusema;

"Nilikuwa napenda kubugia vileo kwa sababu  nilikuwa na msongo wa mawazo, ilifika mahali nikaona ni maisha na mwili wangu naharibu

 

Wakati huo mke wangualikuwa na madharau kwa maana alikuwa anaona vile nilikuwa nalewa, asubuhi nikiingia kazi nalewa, saa saba pia nalewa na hata jioni

Nilijipeleka katika mafunzo yaani rehab ndio niweze kubadilika." Aliongea Omosh.

Huku akizungumzia kwanini wasanii wengi wanapatwa na msongo wa mawazo na kisha wanajiua Omosha alisema.

"Walikuwa wanapokea pesa nyingi, alafu inafika mahali unapata hizo pesa ambazo ulikuwa nazo zimeisha, sasa marafiki wanakutoroka na hautaitwa na marafiki kusheherekea kwa maana huna pesa sasa unapatwa na msongo wa mawazo." 

Omosh alisema kwamba ana wake wawili na amebarikiwa na watoto watano.

Huku akizungumzia kazi ya uigizaji alisema kwamba haina mapato mengi sana.

"Natamani ningekuwa na mtu wa kunipa ushauri wakati ambao nilikuwa napenda pombe kwa maana nimeharibu wakati wangu mwingi sana nikinywa pombe."

Hii hapa video ya mahojiano hayo;