Nachukia kuitwa 'baby mama' wa Bahati-Yvette Obura afunguka

Muhtasari
  • Yvette asema haya kuhusu maisha yake na msanii Bahati na jinsi wanasaidana kumlea mtoto wao
  • Pia alisema kwamba kuna wakati alikejeliwa na wanamitandao huku akijawa na msongo wa mawazo
  • Yvette alisema kwamba hapendi kuitwa baby mama wa mtoto wa Bahati

Leo katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Yvette Obura mama wa mtoto wa msanii Bahati ambaye alizungumzia mambo kadha wa kadha.

Yvette alikuwa katika uhusiano na msanii Bahati na kubarikiwa na mtoto mmoja.

"Mimi nachukia kuitwa baby mama kwa maana huwa naona jina hilo ni ya mtu ambaye anapenda drama ambapo mimi sipendi drama

 

Niliachana na Bahati kwa maana sikuwa nataka kuwa sana kwenye mitandao ya kijamii au wanablogu wala kuwa maarufu niliona hatuwezani

Mimi na Diana tunaheshimiana sana,kwanza wakati mtoto wangu Mueni yuko kwao huwa nazungumza na Diana na wala si Bahati

Diana chenye amenishinda nayo ni kuitwa kewe Bahati." Aliongea Vyette.

Yvette alikana madai kwamba Diana alikuwa katika uhusiano na Bahati alipokuwa na ujauzito wake Bahati.

Pia alisema kwamba kusaidiana kulea mtoto ni jambo nzuri kwa sababu  kila mtu ana mpenzi wake na wameelewana na kuzungumza jinsi ya kumlea mtoto wao.

"Kuna wakati wanamitandao ambao walinikejeli mpaka nikajawa na msongo wa mawazo watu huku nje hawaelewi nini mtu anapitia."

Vyette alisema kwamba hana majuto yeyote baada ya kuachana na Bahati.