Babu Owino ana lipa gharama za matibabu za DJ Evolve hadi sasa-Baba yake DJ Evolve asema

Muhtasari
  • DJ Evolve alivuma kwa muda kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupigwa risasi na mbunge wa Embakasi mashariki
  • Baba yake Elvolve amesema kwamba Babu Owino amekuwa akigharamikia gharama za Evolve licha ya yake kutomuona

Leo kwenye studio zetu tulikuwa naye mcheza Santuri DJ Evolve, ambaye alisimulia jinsi alipata habari kwamba mwanawe yuko hospitalini.

DJ Evolve alivuma kwa muda kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupigwa risasi na mbunge wa Embakasi mashariki.

Bwana Odinda alisema kwamba kabla ya mwanawe kukumbana na ajali hiyo alikuwa amezungumza naye ili wapatane wazungumze mabo kadha wa kadha.

 

"Siku moja kabla ya ajali yake nilimpigia felix simu ni kamwambia aje kuniona,alipokosa kuja kuniona nilijua kwamba amezidiwa na usingizi

Asubuhi nilipokea simu na nikaambiwa niende katika hospitali  kuwa mtoto wangu yuko hosptali, nilipofika Felix alikuwa anaongea na hata kucheka alikuwa anacheka

Baada ya hapo siku iliyofuatia Felix alinyamaza hadi miezi mitano, Babu Owino ndio anasimamia Gharama za DJ Evolve hadi leo,alikuwa anaendelea vyema lakini hivi majuzi amepatwa na shida lakini ,madaktari wanashughulika," Alieleza Baba Evolve.

Pia alisema kwamba Babu Owino hawezi muona mwanawe kulingana na maamuzi ya korti.

"Babu Owino hawezi muona Felix alikatazwa na mahakama, hakuna makubaliano yeyote ambayo tumefanya na Babu ili kutoa kesi yetu mahakamani

Sisi  ni wakristo, na kwa maana tukiomba huwa tunaambia Mungu atusamehe jinsi tunavyo wasamehe hapo ndio tumefungwa

Felix alisema ili apone vizuri hataki mambo mengi kwa hivyo tunapaswa kumsamehe, mwanangu si mtu wa kuongea mengi ni mpole,"