Nilihisi ni mimi nilifanya Azziad akejeliwe baada ya kibao cha utawezana-Femi One

Muhtasari
  • Msanii Femi One azungumzia changamoto alizopitia baada ya kibao cha Utawezana
Femi One
Image: Studio

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye msanii maarufu Femi one ambaye alivuma sana baada ya kutoa kibao cha 'Utawezana' na msanii Mejja.

Baada ya kibao hicho malkia wa tiktoka Azziad alifanya changamoto huku ikiibua mjadala mkali mitandaoni.

Baadhi wa wanamitandao walidai kwamba Azziad ndiye amefanya kibao hicho kuvuma.

Huku akiwa kwenye mahojiano na radiojambo Femi One alisema kwamba baada Azziad kukejeliwa sana mitandaoni alizungumza naye na kumpa mawaidha.

"Kwa sababu ni mimi nilipakia video yake Azziad kwenye mitandao ya kijamii, alipokejeliwa nilihisi ni mimi nimefanya akejeliwe kwa sababu nilipakia video hiyo

Baada ya hapo nilikuwa nazungumza na Azziad, nampa ushauri, nilimuita tukutane lakini alsema kwamba ameshikana

Baada ya mengi kusemwa Azziad aliamua kuninyamzia, lakini najua nilimfikia na tukazungumza," Alisema Femi One.

Msanii huyo alisema kwamba baada ya kutoa albamu yake ana mradi ambao atashirikisha wasanii wa wanawake pekee, hii ni baada ya kuulizwa kama anatarajia kutoa nyimbo na wasanii wa kike.

Pia aliweka wazi kuwa anamchumba, huku akisema kwamba baba yake mzazi aliaga dunia akiwa na miaka 3.

Kwa mahojiano zaidi tembelea, radiojambo youtube.