Mke wangu aliniacha kwa maana nina ugonjwa wa Bipolar-Samuel Boiyo

Muhtasari
  • Samuel Boiyo asimulia jinsi amepambana na ugonjwa wa Bipolar
  • KUlingana na Samuel ugonjwa huo umemfanya apitie changamoto nyingi hata kupelekwa katika hospitali ya watu wenye hawana akili timamu
Samuel Boiyo
Image: Studio

Katika kutengo cha ilikuaje tulikuwa naye Samuel Boiyo ambaye amekuwa akipambana na ugonjwa wa Bipolar kwa miaka 20.

KUlingana na Samuel ugonjwa huo umemfanya apitie changamoto nyingi hata kupelekwa katika hospitali ya watu wenye hawana akili timamu.

"KUna wakati nilienda mpaka ikulu na kuambia watu kwamba nitakuwa rais wa jamhuri ya kenya, ni ugonjwa ambao unakufanya uone kwamba unamakubwa lakini huna chochote 

NImepitia changamoto nyingi ata kuchapwa na polisi na kufungiwa wakina kwuwa mimi ni mhalifu kwani ugonjwa huo ukinipata pia naweza enda kuchukua vitu na bidhaa za watu,"

Samuel pia alisem kwamba mke wake alimuacha kwa sababu ya ugonjwa huo;

"Mke wangu aliniacha kwa ajili ya ugonjwa wa Bipolar, nimeenda mpaka kwao kuzungumza naye ili kumueleza kuwa ugonjwa huu sio wazimu lakini amekataa

NI ugonjwa ambao unachosha mtu na familia yako," Alisema Samuel.

Kulingana na Samuel amekuwa akitumia shilingi elfu kumi kununua dawaa zake, huku akisema kwamba anahitaji msaada kwa maana kuna wakati anakosa pesa za kununua dawa zake na kujipata pabaya.

Pia alisema kuna wakati ugonjwa huo ukimshika anavua nguo zake na kutembea uchi.

Alisema ugonjwa huo unasababishwa na jambo ambalo mtu alipitia na kupatwa na mshtuko, au ni jambo la familia ambao mtu huzaliwa nalo.