Nilifukuzwa na wazazi wangu na kuishi msituni nikiwa darasa la 4-Eric Mkabwa

Muhtasari
  • Leo kwenye kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Eric Mkabwa ambaye alitengwa na familia akiwa katika darasa la nne baada ya kaka yake kuaga dunia
Eric Mukabwa
Image: Studio

Leo kwenye kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Eric Mkabwa ambaye alitengwa na familia akiwa katika darasa la nne baada ya kaka yake kuaga dunia.

Kulingana na Eric jamii yake ilisema kwamba ni yeye alimuua kaka yake, na kisha akafukuzwa nyumbani na kuenda kuishi na wanyama.

"Kaka yangu aliaga dunia baada yetu kupata tohara, baada ya kutahiriwa kaka yangu alianza kupigana na binamu yangu

Ili kuwatenganisha kaka yangu alikuwa na kijiti, alikuwa anarushia binamu yagu niligonga kijiti hicho na kugonga kaka yangu kwenye sehemu za siri

Alipelekwa hospitali baada ya siku chache aliaga dunia na lawama yote ikaekelewa kwangu kwamba ni mimi nimemuua kaka yangu

Sikupewa nafasi ya kujieleza wala kaka yangu hakupewa nafasi ya kueleza nini haswa kilitokea,nilifukuzwa na nikaenda kuishi na wanyama msituni, wakati huo marafiki zangu wa karibu walikuwa ndege, na wanayama wa msituni," Alieleza Eric.

Je baba yake alikuwa na yapi ya kusema kuhusu tukio hilo?

"Nakubuka baba yangu akija msituni na kuniambia nisijali, kwa sababu watanituma Mombasa au Kisumu kama ishara ya kuhadhibiwa kwa kumuua ndugu yangu

Shangazi wangu walikuwa wakiniona wanawaambia watoto wao wajifiche kwani mimi nimuuaji, nilikuwa naia kila siku kwa ajili ya hayo

Sijawahi juta , kwa maana ndugu yangu alikuwa ananikujia ndotoni na kunipa motisha na kunitia moyo."

Je wazazi wake walimsamahe na uhusiano wao uko vipi?Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube