'Bado ninamuomboleza mwanangu,'Mama yake Sharon Otieno asema

Muhtasari
  • Mamake Sharon Otieno asema bado anaomboleza kifo cha mwanawe
Melida Otieno
Image: Studio

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye Melida Otieno, mamake Sharon Otieno aliyeuliwa kinyama, Ilidaiwa kwamba Sharon alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na gavana wa Migori Okoth Obado 

Huku akizungumzia mauaji ya mwanaee alisema kwamba ana machungu, na bado anamuomboleza mwanawe kwani alikuwa nguzo ya familia.

"Sharon alikuwa anapenda masomo, alikuwa mwenye furaha na alipenda maendeleo. Ninampeza sana kama mwanangu wa kwanza na kwamba alikuwa nguzo, nguzo ya masomo yake. Bado tuna machungu... Bado ninamuomboleza," Alizungumza Melida.

Melida alidai kwamba baada ya kujua kuwa mwanawe ana uhusiano na gavana Obado, alimuonya kuhusu uhusiano wao.

"Nilikuja kujua baadaye kwamba Sharon alikuwa na uhusiano na Obado ila sitazungumzia maanake ni jambo ambalo liko kortini. Nilihisi vibaya kuwa ana uhusiano naye na nilimwambia ila alikuwa ni mtu mzima..."

Wiki iliyopita Melida alidai kwamba anataka kujiunga na siasa, na akizungumzia hayo alisema kwamba atawania wadhifa wa wakilishi wa wanawake kwani wanawake wanapitia changamoto nyingi.

"Mimi nilizaliwa mwanasiasa. Nilisukumwa na jamii ili niiwakilishe... Sidhani nilipata umaarufu kufuatia kifo cha mwanangu... Sina 'godfather' katika siasa

Nataka kuingia katika siasa. Nilikuwa ninataka kuwania wadhifa wa uwakilishi wadi ila sasa ninataka kuwania kama mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Homa Bay kufuatia mahitaji ya umma ili niwakilishe hasla... Wanawake wanapitia changamoto sana,"Melida aliongea.

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.