Sikuwa 'informer' wa sonko, amekuwa akinitishia-Merry Nkatha hatimaye azungumza

Muhtasari
  • Alidai Sonko amekuwa akitaka kuwa shahidi wake katika kesi mbili dhidi ya Gavana Anne Kananu na Jaji Saidi Chitembwe miongoni mwa kesi zingine
  • Akizungumza na Radiojambo, Nkatha amedai kwamba hajawahi mpa Sonko habari za siri
Image: FACEBOOK// MIKE SONKO

Baada ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko kumgeukia mwanamke ambaye alitaka ulinzi wa polisi kutokana na vitisho vya gavana huyo wa zamani, hatimaye Merry amefunguka haswa nini kilitendeka kati ya wawili hao.

Merry Nkatha alienda katika kituo cha polisi cha Karen kutafuta ulinzi akisema anahofia maisha yake. Alisema anahofia Sonko au maajenti wake wanaweza kumdhuru kwa kukataa kushirikiana naye.

Alidai Sonko amekuwa akitaka kuwa shahidi wake katika kesi mbili dhidi ya Gavana Anne Kananu na Jaji Saidi Chitembwe miongoni mwa kesi zingine.

Akizungumza na Radiojambo, Nkatha amedai kwamba hajawahi mpa Sonko habari za siri.

"Kitu cha kwanza naweza sema kwamba sijawahi kuwa 'informer' wa Mike sonko,alikuwa anataka niwe shahidi katika kesi zake lakini nilikataa, apo ndipo alinipa milioni 250 lakini nilikataa

Baada ya kukataa aliamua kusambaza video za uongo, ukweli ni kuwa video zake zimehaririwa na wala si za kweli, amewahusisha watu wengi

Kama mimi ni rafiki yake kwa nini anajaribu kuharibu jina langu, ina maana kuna kitu nimekataa kufanya ili afanye hatua hiyo," Nkatha aliongea.

Aidha Merry amedai kwamba Sonko amekuwa akimtishia, na hata alishikiwa bunduki na wanaume 3 na kuripoti kisa hicho kwa polisi.

"Sio mara ya kwanza kushikiwa bunduki, na nimeripoti kwa polisi, Sonko amekuwa akinitishia na ata watu wangu, ni kama amekuwa akinieka kifungo cha nyumbani

NInahofia maisha yangu ndio maana nilitoka kwangu na kukaa kwenye niko sasa hivi, nina watoto ambao wako shuleni sijui usalama wao au wanafikiria nini

Mimi sio mtu wa kwanza kutekwa nyara na Sonko ni watu wengi sana ata wawakilishi wadi," Alisema Nkatha.

Radio Jambo Kenya | Ongea Usikike | Ni kituo nambari moja Kenya kwa matangazo ya kiswahili. Vipindi vyake vina jumuisha Spoti,Mijadala moto moto na muziki wa Kiafrika #RadioJamboKenya Subscribe to RadioJambo Youtube - https://bit.ly/39wwc6u Mitandao ya Kijamii Instagram - https://rb.gy/e154d1 Facebook - https://rb.gy/09d1b9 Twitter - https://rb.gy/e23220