Mpenzi wangu aliniambia mama yake ameaga dunia, kumbe ni uongo-Asimulia Mwanamume

Muhtasari
  • Mwanamume asimulia jinsi alitendwa na mpenziye, baada ya kugundua amekuwa akimdanganya

Mwanamke anaweza fanya lolote au chochote kwa ajili ya mapenzi lakini haiwezi vuka mipaka na kuua mtu ambaye yuko hai.

Katika kipindi cha mbusi na lion tejeteke mwanamume mmoja alitaka aliyekuwa mpenzi wake apigwe nyahunyo baada ya kumdanganya kuwa mama yake ameaga dunia.

Pia alimkula pesa na hata kumwaribia jina kwa majirani.

 

Huu hapa usimulizi wake;

"Mimi nataka aliyekuwa mpenzi wangu apigwe nyahunyo, hii ni kwa sababu alinidanganya kuwa mama yake ameaga dunia lakii mama yake yuko hai

Nilichunguza na nikapata mama yake yuko hai, baba yake ni muhubiri, kuna wakati alipotoka kwangu aliniambia anataka kurudi nimtumia nauli, nilipomtumia hakukuja

Baada ya muda alinipigia simu akiwa na binamu zake kuwa amevunjika mguu, nikamtumia pesa kumbe ilikuwa uongo hakuwa ameumia

Pia aliniharibia jina kuwa siwezani na mambo ya kitandani, aliambia majirani mpaka nikahama," Mwanamume huyo alisimulia.