Nyahunyo:Rafiki yangu alimwambia mpenzi wangu kuwa mimi ni chokora

Muhtasari
  • Rafiki yangu alimwambia mpenzi wangu kuwa mimi ni chokora
Mbusi na Lion

Katika kitengo cha nyahunyo jamaa mmoja alitaka rafikiye apewe nyahunyo kwni amekuwa akimtusi mbele ya mpenzi wake.

Jamaa huyo kutoka Kitale alidai kwamba rafiki yake ana mazoea ya kumtusi mbele ya mpenzi wake kwa maana anauza dania sokoni.

"Nataka rafiki yangu apewe nyahunyo, kwa sababu ana mazoea ya kunitusi baada ya kuniona na mpenzi wangu

Mimi ni muuzaji dania katika soko la kitale naye ni mwendesha boda boda, kuna wakti alimwmbia mpenzi wangu kuwa mimi ni mwendawazimu, na pia mimi ni chokora

Ananidharau kwa maana nauza dania," Alieleza.

Kweli hawakukosea walipoimba kwaba kazi ni kazi, bora tu ujikimu na kisha upate mkate wa kila siku.

Je una rafiki yako ambaye amekuwa akikuchomea mbele ya marafiki au mpenzi wako, kwani hayo ndiyo mazoea yao.