Nyahunyo:Jamaa achapwa nyahunyo kwa kuenda haja ndogo kwenye gari lake

Muhtasari
  • Jamaa achapwa nyahunyo kwa kukojolea gari lake
Mbusi,DJ Nyc na LIon
Image: Radiojambo

Wakifanya tabia mbaya tunawachapa,upuzi tuna chapa,uzembe na upuzi tunachapa nyahunyo hata makosa tuna chapa nyahunyo kwenye kitengo cha nyahunyo.

Siku ya Jumanne jamaa moja ambaye anafanya kazi ya kuosha gari, alitaka mteja wake achapwe nyahunyo kwa ajili ya tabia ambayo amekuwa akifanya kwa muda mrefu.

Kulingana na mwanamume huyo amekuwa akienda haja ndogo kwenye chupa na kutupa kwenye gari lake wakati anapopeleka ikaoshwe.

"Nataka mtej wangu ambaye ana mazoea mabaya achapwe nyahunyo anatabia ya kukojolea chupa na kuweka kchini ya gari yake tunaona tunapoanza kuosha gari lake

Ni tabia ambayo amekuwa akifanya kwa muda mrefu, kisha anatuambia apate gari lake limeng'ara, sio tabia ya kupendeza wala ya kufanywa na mtu ambaye amekomaa."

Je jamaa huyo alikuwa na maosa ua la?