PATANISHO:Niliachana na mke wangu baada ya kunipata na mpango wa kando

Muhtasari
  • Baada ya mke wangu kunipata na mpango wa kando nami nikampata mpango wangu wa kando na mwanamume mwingine
  • Kazi ya mume wangu alikuwa anakaa tu nyumbani nifanye kazi na kuwapeleka wanawake kwa mama yake wanasheherekea kwa maana mimi ndio nilikuwa ndume wa nyumba
  • Kama anataka turudiane alete ng'ombe kwetu
Gidi na Ghost
Image: Radiojambo

Katika kitengo cha patanisho hii leo bwana Sylvester alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe waliokosna naye miaka nne iliyopita baada ya kumpata na mwanamke mwingine.

"Nilikosana na mke wangu baada ya kunipata na mwanamke mwingine,mke wangu alikuwa akifika nyumbani ananiambia amechoka

Tulikuwa tumebarikiwa na watoto wawili lakini mmoja aliaga dunia, baada ya kunipata na mwanamke huyo baada ya muda nilimpata mpango wangu wa kando na mwanamume mwingine pia." Alieleza Nyongesa.

 

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumpigiwa mkewe Nancy alikuwa na haya ya kusema,

"Huyu mwanamume alikuwa ameniletea mwanamke mwingine alafu ananiambia kuwa ameniletea mwanamke mwingine mwenye kiuno kikubwa kama changu

Nimekuwa nikimlisha mwanamume huyo tangu anioe alikuwa tu anioe kwa ajili ya ngono na si kitu kingine

Ilifika wakati yeye anakaa tu kwa nyumba namlisha namuachia kila kitu kwa nyumba mpaka mahali alifika akasema hatawahi kula mboga anataka mayai nafanya juhudi zangu namuachia kila kitu lakini anapelekea wanawake wengine pesa zangu

Pia alikuwa anawapeleka wanawake kwa mama yake wanakula, na kusheherekea kwa maana ni mimi nilikuwa ndume wa nyumba, kama anataka turudiane haya basi alete ng'ombe beberu kwa maana nimezaa na wao." Alisema Nancy.

Kwa mwengi zaidi tembelea mitandao ya kijamii ya youtube ya Radio jambo.