Patanisho:Wakwe zangu walinikataa nilipoenda kutambulishwa kwao na kuniita 'slayqueen'

Muhtasari
  • Nilifukuzwa kwangu na shangazi wa mume wangu
  • Wakwe wangu walinikataa nilipoenda kutambulishwa kwao na kuniita 'slayqueen'
Gidi na Ghost

Leo katika kitengo cha patanisho Bi. Rahab alituma ujumbe ili apatanishwe na wakwe wake hasa nduguye mkwe ambaye alimtusi.

Huu hapa usimulizi wake Rahab;

"Nilipelekwa na mume wangu kwao ili aweze kunitambulisha kwa wakwe wangu nilipofika ni kama hawakunipenda

 

Nilipomuuliza mume wangu aliniambia kuwa niweke amani kati yangu na watu wa kwao, aliniambia kuwa nilikuwa naamka saa tatu ndio maana sipendwi kwao

Pia si kuwa nala chakula yao kwa maana ninaugonjwa wa sukari, tuliporudi ndugu ya mume wangu alimpigia simu na kumwambia aniwache

Shangazi yake ndiye alinifurusha kwa mume wangu sasa niko kwetu." Alieleza Rahab.

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumpigia ndugu ya mume wake alikuwa na haya ya kusema.

"Mimi sitaki ujinga wake akae." Alisema ndugu huyo na kisha akakata simu.

Rahab kwa huzuni mwingi alitoa machozi huku akisema kwamba ana ujauzito ilhali mumewe hayuko katika upamde wake bali upande wa wazazi wake.

Kwa mengi zaidi tembelea radiojambo youtube.