Patanisho:Mke wangu aliniacha baada ya kupooza upande mmoja

Muhtasari
  • Katika kitengo cha patanisho bwana David  Thuo alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe aliyekosana naye mwezi uliopita baada yake kuwa mgonjwa mwaka jana
Gidi na Ghost

Katika kitengo cha patanisho bwana David  Thuo alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe aliyekosana naye mwezi uliopita baada yake kuwa mgonjwa mwaka jana.

"Nilikosana na mke wangu baada yangu kuwa mgonjwa na kupooza mwaka jana, nadhani aliniacha kwa maana sikuwa najukumikia mahitaji kama mwanamume

Nimejaribu mbinu zote lakini aliniambia hawezi nirudia, tumebarikiwwa na mtoto mmoja,"

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumfikia mkewe, alisema kwamba hatamrudia mumewe kwani alimuumiza moyo.

"Kama nikumuacha ningemuacha mapema akiwa hospitalini, lakini baada yake kupata nafuu alianza kuniita kuwa mimi ni malaya

Mimi sirudi, kwa sababu alinionyesha madharau, kaika ndoa yetu amekuwa akimsikiliza mama yake kuniliko,waha mama yake amsaidie vile alikuwa anasema atamsaidia

Msimamo wangu wa mwisho ni kuwa sirudiani naye," Wambui alisema.