- Niko tayari kuwa na wake wenza kuliko mume wangu kuhanya
Katika kutengo cha patanisho Everlyne alituma ujumbe ili apatanishwe na mume wake Daniel baada ya kumfumania na mwanamke mwingine wakiwa uchi.
Kulingana na mwanamke huyo wamekuwa pamoja kwa miaka saba na wamebarikiwa na watoto 4 na anatarajia mwingine mwezi ujao.
"Naomba mnipatanishe na mume wangu wa miaka 7. Nilimfumania na mwanamke mwingine jana wakiwa uchi na hajasema lolote. Nina watoto wanne na ninatarajia mwingine mwezi ujao
Mwanamke huyo amekuwa akinitumia jumbe akinitusi, nimekuwa nikilia sana katika ndoa yangu, nikimuuliza amekuwa akiniambia kwamba niache kufuata maisha yake
Nataka tupatanishwe anaiambie ama kuna mahali huwa nakosea, nilipowafumania hakurudi nyumbani, niko tayari kuwa na wake wenza ata kama ni saba kuliko atoke nje ya ndoa," A;isema Everlyne.
Baada ya kufanya juhudi za kumpigia mumewe simu hakupatikana,je ni ushauri upi unaweza mpa Everlyne kwa yote amekuwa akipitia.