Patanisho: "Mamangu wa Kambo alileta mganga wakapeperusha kuku, nikaanguka" Kijana afunguka

Allan alisema alijiskia sawa baada ya kutojielewa siku nne.

Muhtasari

•Alisema kwamba alizozana na Bi Doreen kutokana na hasira kabla ya kumtumia meseji ambazo hazifai.

•"Alileta mganga mchana wakapeperusha kuku nikiona, Waliikimbiza wakashika. Mganga huyo alikuwa mwanaume mrefu . Hakuwa amevaa chochote mguuni. Nilijiskia nikiwa sawa baada ya siku nne," Allan alisema.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha Patanisho kwenye Gidi na Ghost Asubuhi,  Allan Wabwire mwenye umri wa miaka 19 kutoka kaunti ya Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mamake wa Kambo, Bi Doreen.

Allan alidai kuwa uhusiano wake na mamake ulivunjika takriban miaka miwili iliyopita kufuatia ugomvi wa nyumbani.

Alisema kwamba alizozana na Bi Doreen kutokana na hasira kabla ya kumtumia meseji ambazo hazifai.

"Mwaka wa 2019, mwezi Novemba. Nilikuwa form 2 nikarejea nyumbani. Mama alikuwa ameweka mbegu ya mboga bila hiari yake nikaenda nikapanda. Alikuja kugundua baada ya mbegu kumea akaanza kunigombanisha. Nilimpigia baba nikamuomba niende nikaishi na shangazi yangu hadi tufungue shule," alisimulia.

Alisema kwamba baba yake alimruhusu aende kwa shangazi yake na alirejea tu wakati babake aliporudi Bungoma.

Allan alifichua kwamba alizozana tena na mamake mwaka wa 2020 wakati mzozo ulitimbuka kati yake na jirani. Alidai kufuatia hayo, mke huyo wa babake alimuita mganga nyumbani ili amshughulikie.

"Wakati wa corona nikarudi nyumbani. Mama aligombana na jirani ikawa sababu ni mimi. Alinipeleka kwa mganga akaniharibu kichwa. Niliona mganga akakuja akapeperusha kuku na damu kisha nikaanguka

Alileta mganga mchana wakapeperusha kuku nikiona, Waliikimbiza wakashika. Mganga huyo alikuwa mwanaume mrefu . Hakuwa amevaa chochote mguuni. Nilijiskia nikiwa sawa baada ya siku nne," alisema.

Alieleza kwamba baada ya babake kurejea nyumbani tena alishughulikiwa akawa sawa.

Allan alisema kuwa baba yake amekuwa akimshauri awe na uhusiano mwema na mamake wa kambo ila hilo limekuwa ngumu kutimia.

Bi Doreen alipopigiwa simu alisema kwamba hajawahi kukosana na mtu kisha akakata simu mara moja.

"Sijawahi kukosana na mtu!" alisema.