Patanisho: Jamaa aonyeshwa upendo na mama mkwe baada ya kupatanishwa

"Sisi tuko tayari kusuluhisha kama wazazi. Kuja nyumbani tuongee," Bi Emily alisema.

Muhtasari

•Mariko alisema uhusiano wake na mama mkwe wake ulisambaratika baada ya kumzuia mkewe kuenda nyumbani.

•Mariko aliweka wazi kwamba alitaka tu kujua ikiwa mke wake yuko nyumbani ndio ajue hatua bora ya kuchukua.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Mariko Omondi kutoka Kawangware alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mama mkwe wake Emily Naswa.

Mariko alisema uhusiano wake na mama mkwe wake ulisambaratika baada ya kumzuia mkewe kuenda nyumbani.

"Wakati mama yake alinipigia akaniambia anataka msichana aende nyumbani, nilikataa juu sikuelewa kwa nini alitaka aende. Nilimwambia asiende kwanza mpaka niende nyumbani," alisema.

Aidha alifichua kwamba mkewe alitoroka na hajui aliko.

"Nimepigia mama yangu akaniambia hayuko nyumbani. Ni kama ametoka kwetu. Nilikuwa nampea pesa za matumizi. Simu yake imezimwa.Sijaelewa mahali msichana yuko. Mama mkwe hashiki simu zangu,"

Mama Emily alipopigiwa simu alimuuliza Mariko kwa nini alikimbilia kupatanishwa kabla ya kufika nyumbani kwao.

Mariko hata hivyo alisisitiza kuwa Bi Emily hajakuwa akishika simu zake.

"Mimi sijawahi kukataa kushika simu yako. Nimetoka kuchukua dawa, Precious ni mgonjwa, ameumwa na tumbo usiku," alisema.

Aliongeza,"Mambo yangu na baba yake unafaa tu ukuje nyumbani. Ukiwa mbali hivyo na unaulizia Medrin tutajuaje unataka mke wako?"

Mariko aliweka wazi kwamba alitaka tu kujua ikiwa mke wake yuko nyumbani ndio ajue hatua bora ya kuchukua.

Bi Emily alifichua kuwa shemeji huyo wake alidaiwa kuoa mwanamke mwingine baada ya kutangena na binti yake.

"Medrin ako mzima, angekuja nyumbani aongee na wazazi. Walikosana miaka miwili iliyopita. Kijana alifika mahali akachukua msichana mwingine. Yeye akuje tu aongee waelewane," alisema.

Kufuatia hayo, Mariko alimwomba mama mkwe wake ashike simu zake wakati atakapompigia.

"Jaribu kumwambia Medrin kama kuna kosa anisamehe," alisema.

Bi Emily alisema, "Sisi tuko tayari kusuluhisha kama wazazi. Kuja nyumbani tuongee,"