Patanisho: "Wakizaa watoto tutaitana aje!" Mzee amlilia bintiye baada ya kuolewa na ndugu yake mdogo

"Kila wakati ndugu yangu alikuwa anashinda na huyo mtoto. Nikimuuliza kwa nini, alikuwa ananiambia anafanya guidance and counselling," Bw Simiyu alisema.

Muhtasari

•Bw Simiyu alisema binti yake aliacha shule na kuenda kuolewa na jamaa ambaye anapaswa kuwa mjomba wake.

• Asiola ni ndugu yangu wa mama mdogo, sasa wewe na Asiola mkizaa mtoto, tutaitana aje  na wao?" Bw Simiyu alimlalamikia bintiye.

Image: RADIO JAMBO

Mzee aliyejitambulisha kama Benard Simiyu ,57, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na binti yake Mebo Simiyu ,20, ambaye alikosana naye takriban miaka minne iliyopita kufuatia mzozo wa kifamilia.

Bw Simiyu alisema uhusiano wake na binti yake uliharibika mwaka wa 2020 wakati ambapo mwanadada huyo aliacha shule na kuenda kuolewa na jamaa ambaye anapaswa kuwa mjomba wake.

Alisema jamaa ambaye alimuoa bintiye ni ndugu yake, ambaye ni mtoto wa mamake mdogo.

"Huyu msichana wangu alikuwa na miaka 16, alikuwa kidato cha pili... Ndugu yangu mdogo alikuwa amekuja 2019 wakati babangu alikufa, alikuwa na miaka 22. Alikuja akiwa na rasta na tukamkubalina tukampatia shamba.

Alafu alichukua mtoto wangu wa miaka 16 akampachika mimba, na akamuoa. Nilifuatilia kisha tukachukua mtoto tukamrudisha shule. Baadaye alikuja akamtoa shule, sasa hivi wanaishi kama mume na mke," Bw Simiyu alisimulia.

Bw Simiyu aliweka wazi kwamba licha ya makosa ya bintiye, tayari amemsamehe na angependa arejee ili wamrudishe shule.

"Hata tulikuwa tumeshtaki huyo jamaa na kesi ya unajisi. Mimi nishawasamehe lakini msichana wangu arudi aendelee na shule. Binti yangu huenda anaogopa kurudi anadhani kama familia tutampiga lakini mimi nishamsamehea," alisema.

Mebo alipopigiwa simu alisema, "Niliwaambia nitakuja nyumbani. Sina shida na wao. Nitakuja mwezi wa nane" kisha akakata simu.

Bw Simiyu aliendelea kumlalamikia bintiye akimueleza kwamba hafai kuwa kwenye ndoa na jamaa ambaye alimuoa kwani ni ndugu yake.

"Mimi ninakutambua kama mtoto wangu. Wewe unajua makosa ambayo ulifanya. Asiola ni ndugu yangu wa mama mdogo, sasa wewe na Asiola mkizaa mtoto, hao watoto tutaitana aje  na wao?" Bw Simiyu alimwambia bintiye.

Aliendelea kusema, "Huyo Asiola tulimpa shamba ekari moja. Kila wakati ndugu yangu alikuwa anashinda na huyu mtoto. Nikamuuliza kwa nini huwa anashinda na msichana mdogo. Alikuwa ananiambia anafanya guidance and counselling. Nikamuuliza kwa nini hiyo guidance and counselling hawafanyii wavulana ilhali niko na watoto wavulana."

"Mwaka wa 2022, nilimchukua mtoto nikampeleka hadi shule. Msichana alisema kama sio huyu ndugu yangu, hawezi kuolewa na mwingine. Sasa wakizaa watoto tutaitana aje na wao. Na huyo Asiola atafute bibi! Walitoroka, nikawafuata na pikipiki hadi ikaisha mafuta. Huyo jamaa aache mtoto bana," alisema kwa uchungu.

Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?