Patanisho: "Sina muda na yeye, anisahau kabisa!" Mwanadada amkataa mumewe

Tulivurugana kwa muda alafu nikamchapa kofi kidogo," Shikuku alisema.

Muhtasari

•Shikuku alisema mkewe aligura ndoa yao ya mwaka moja wiki jana baada ya wao kuhusika katika mzozo wa nyumbani.

•Catherine hakuficha hasira yake dhidi ya mumewe na akaweka wazi kuwa hakutaka kuzungumza naye.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho, Leonard Shikuku (28) alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Catherine (22).

Shikuku alisema mkewe aligura ndoa yao ya mwaka moja wiki jana baada ya wao kuhusika katika mzozo wa nyumbani.

"Wiki jana aliniambia anataka kuenda nyumbani kwao. Kwa kuwa mfuko yangu ilikuwa chini nikamwambia ataenda siku ingine. Tulivurugana kwa muda alafu nikamchapa kofi kidogo," alisema.

Shikuku alisema baada ya kumpiga mkewe alikasirika na kutoroka nyumbani kwao.

"Alienda pekee yake alafu akatumana mtoto akujiwe. Sasa hivi nikipiga simu ananiongelesha kwa madharau,"

Catherine alipopigiwa simu hakuficha hasira yake dhidi ya mumewe na akaweka wazi kuwa hakutaka kuzungumza naye.

"Sina muda na yeye. Anisahau kabisa!" alisema kabla ya kukata simu.

Shikuku alipopatiwa fursa ya kuomba msamaha hewani alimuomba mkewe kuelewa sababu yake kutompatia nauli ya kuenda kwao.

"Wakati mwingine mtu anaweza kuwa hana kile unataka lakini ana nia ya kusaidia. Nisamehe tu na turudiane tulee mtoto wetu," alisema.

Gidi na Ghost walimshauri ampatie mkewe muda wa kupunguza hasira.