Nilipata mpango wangu wa kando ni mpenzi wa baba yangu-Mwanamume afichua haya

Muhtasari
  • Mwanamume mmoja asimulia jinsi wanakula chakula kimoja na baba yake kutoka kwa mpango wao wa kando
sad man
sad man

Mwanamume mmoja aliwaacha mashabiki wa Radiojambo midomo wazi baada ya kutoboa siri yake huku akisema imemletea shida.

Mwanamume huyo ambaye ni baba wa watoto watatu alisema kwamba alikuwa na mpango wa kando ambapo aligundua kuwa kipusa huyo ni mpenzi wake baba yake.

"Nina familia mke na watoto watatu, nilikuwa na mpango wa kando ambapo tumekuwa naye kwa muda baada ya muda niligundua kuwa ni mpenzi au mpango wa kando pia wa baba yangu

 

Mwanamke huyo alienda kumwambia baba yangu kuwa amepata mpenzi ambaye anataka amuoe, baba yangu ameleta shida sana kwa maana anataka kuona mtu huyo ambaye ni mimi

Mwanamke huyo hajui kwamba huyo ni baba yangu, na baba yangu hajui kwamba mwanamume huyo ni mimi kwa hivyo anataka kuniona

Mpango huyo wa kando aliniambia kwamba ni mimi anataka na wala si baba yangu na anataka kuenda kunitambulisha ili baba yangu aone yuko na mpenzi." Alieleza Mwanamume huyo.

Je unaweza mpa ushauri upi mwanamume huyo, na ukieza gundua kwamba baba yako ni mpenzi wa mpango wako w kando utafany aje?