Nilitumia akaunti feki ya facebook kula 'fare' ya wanaume nikiwa na mpenzi wangu-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Mwanamume atoboa siri jinsi amekuwa akila 'fare' ya wanaume
  • Kumbe sio wanawake tu wanajua kuwatapeli wanaume, lakini wanaume wameingia katika mkondo huo wa kutapeli
Lion,DJ Nyce na Mbusi
Image: Studio

Kumbe sio wanawake tu wanajua kuwatapeli wanaume, lakini wanaume wameingia katika mkondo huo wa kutapeli.

Katika kipindi cha Mbusi na Lion kitengo cha Toboa Siri mwanamume mmoja alitoboa siri jinsi aliwatapeli wanaume akiwa na mpenzi wake huku wakitumia akunti feki ya facebook.

Huu hapa usimulizi wake;

 
 

"Nilifungua akaunti ya facebook, na kuweka picha ya mwanamke, nilimjulisha mpenzi wangu, tumekuwa tukikula pesa za wanaume wakituma ili nipatane na wao

Wakipiga simu mpenzi wangu ndiye alikuwa anazungumza na wao kisha wanatuma fare, 

Siku moja ndugu yangu alinipigia simu akifira amepigia mwanamke huyo wa facebook, nilimpa mpenzi wangu wakazungumza lakini nikamwambia kwamba huyo ni ndugu yangu

Aliniambia wacha tumchanue, sasa mpenzi wangu amekuwa mpenzi wa ndugu yangu, nataka kutoboa siri niwaambie kwamba akunti hiyo ni yangu wala sio ya mwanamke

Pia nataka kumtobolea ndugu yangu ni mwambie kwamba huyo mpenzi wake alikuwa mpenzi wangu na tulikuwa tunakula pesa za nauli za wanaume," Alisimulia.

Haya basi wanaume mmefunzwa somo wacheni kutuma fare ovyo ovyo, na kwa upande mwingine mwanamume pole kwa ndugu yako kunyakuwa mpenzi wako ulipenda pesa sana.