Mke wangu anafahamu mpango wangu wa kando ni mteja wangu-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Zikiwauma huwa wanamwaya mtama kwa mashabiki wa radiojambo wakati wa kipindi cha toboa siri
Lion na dj Narty
Image: Studio

Zikiwauma huwa wanamwaya mtama kwa mashabiki wa radiojambo wakati wa kipindi cha toboa siri.

Sio wote huwa wanajigamba lakini huwa na siri za kutoboa siri ambazo huwashtua wengi na hata kuwaacha wengi midomo wazi.

Mwanamume mmoja alitoboa siri jinsi mpango wake wa kando amekuwa akimsumbua baada ya ujauzito wake.

Kulingana na mwanamume huyo, mpenzi wake amekuwa akimpigia siymu nyakati za usikuakiwa na mkewe.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nilipata mpango wa kando mke wangu akiwa nyumbani, tulifanya tendo la ndoa kisha akabeba ujauzito wangu

Baada ya muda mume wake alijua kwamba ujauzito sio wake,na akamfukuza mpango wangu wa kando, sasa amekkuwa akinisumbua kwa simu ananipigia simu na niko na mke wangu ambaye alirudi 

NImekuwa nikimdanganya mke wangu kuwa mwanamke huyo ni mteja wangu, kwa maana nafanya kazi ya mabomba

Nataka wanajambo wanishauri kama nimwambie mke wangu siri hii, ama nikuwe nikimsaidia mpango wangu wa kandokama hajui," Alieleza mwanamume huyo.