Kuna mama ameniweka licha ya kuwa na mke nyumbani-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama katika kitengo cha toboa siri, jamaa mmoja ametoboa siri jinsi amekuwa akiekewa na wanawake baada ya kuja Nairobi
  • KUlingana na mwanamume huyo, alipatana na mama ambaye anafahamika mama Kanini, na alimueka
DJ Slim,Mbusi na Lion
Image: Studio

Kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama katika kitengo cha toboa siri, jamaa mmoja ametoboa siri jinsi amekuwa akiekewa na wanawake baada ya kuja Nairobi.

KUlingana na mwanamume huyo, alipatana na mama ambaye anafahamika mama Kanini, na alimueka, baada ya muda alipatana na mwanamke ambaye ni daktari na amemueka vyema kumliko mama Kanini.

Siri

"Nilikuja Nairobi kutafuta kazi, nilipatana na mama anaitwa mama Kanini lakini niliachana naye na nikachukuliwa na mama ambaye ni daktar na gari

Mwanamke huyo anafahamika kama Halima, lakini Mama Kanini amekuwa akinipigia simu usiku nikiwa na Halima na amesema kwamba atamgonga na gari asiponiwacha

Nina bibi nyumbani ambaye amekuwa akitumiwa pesa na Halima, nataka kumtobolea Mama Kanini siri ni mwambie simtaki, kwa maana hakuwa ananisaida ilhali nilikuja Nairobi kutafuta pesa," Alisema Jamaa huyo.

Makubwa haya, je maoni yako kwa ajili ya mwanamume huyu ni yapi?