Mwajiri wangu anajua mimi ni kijakazi, kumbe mimi ni mke mwenza wake-Kipusa atoboa siri

Muhtasari
  • Kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama,kipusa mmoja aliwaacha mashabiki wa radiojambo mdomo wazi baada ya kufichua siri kuwa yeye sio kijakazi bali mke mwenza
Lion,DJ Nyce na Mbusi
Image: Studio

Kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama,kipusa mmoja aliwaacha mashabiki wa radiojambo mdomo wazi baada ya kufichua siri kuwa yeye sio kijakazi bali mke mwenza.

Kulingana na kipusa huyo mpenzi wake alimpeleka kwake kama kijakazi, ilhali mwajiri wake hajui kwamba ni mke mwenza wake.

Pia alisema kwamba amebarikiwa na mtoto mmoja na mwanamume wa nyumba hiyo, lakini mkewe hajui chochote.

Hii hapa siri yake;

"Nilikuwa na mpenzi licha ya kumkubali nilifahamu kwamba ana mke, tuliamua anipeleke kwake kama kijakazi lakini chini ya maji mimi ni mke mwenza

Mwajiri wangu mwanamke hajui kwamba mimi ni ke mwenza, ata amekuwa akiniibia siri kwamba mumewe hana haja na haki ya kitandani

Nina mtoto mmoja na mwajiri wangu na anawafanana na watoto wake, ilhali mkewe hajawahi jua kwamba mtoto huyo ni wa mume wake

Aliponiuliza mtoto ni wa nani nilimdanganya kwamba ni wa mwanamume mwingine ili asijue siri yangu na mumewe

Pia nilimdanganya mwanamume huyo mwingine kwamba mtoto ni wake, na amekuwa akinitumia pesa za kumtunza mtoto wangu

Siku ya jumapili huwa tunaenda na mpenzi wangu kwenye vyumba vya kulala, tunamaliza mambo yetu kisha nina rudi kazini," Alitoboa mwanamke huyo.

Je mwanamke huyo anastahili kutoboa siri hiyo au akanyagie?