Nilirogwa na mama wa kambo nisiwahi rudi nyumbani-Jamaa amtobolea baba yake siri

Muhtasari
  • Katika kitengo cha toboa siri, jamaa mmoja aliwaacha mashabiki wa radiojambo, na hisia tofauti baada ya kutobia siri kwamba alirogwa na mama yake wa kambo
(Kushoto) Mbusi (kati) DJ Nyce (kulia) Lion
Image: Studio

Katika kitengo cha toboa siri, jamaa mmoja aliwaacha mashabiki wa radiojambo, na hisia tofauti baada ya kutobia siri kwamba alirogwa na mama yake wa kambo.

KUlingana na jamaa huyo, alitabiriwa kwamba alirogwa na uzi wa sweta, mfuko wa shati lake la shule na kaptura.

Pia alifichua kwamba kiini kubwa cha kurogwa na amamyake ni kuwa asiwahi rudi nyumbani, na endapo atarudi ataaga dunia.

Hii hapa siri yake;

"Nataka kumtobolea baba yangu mzazi, sababu kuu ya kutorudi nyumbani ni kwa ajili mke wake yaani mama yangu wa kambo aliniroga

Mama yangu mzazi aliaga dunia,nilitabiriwa kwamba  alinirofa na kaptura yangu ya shule, uzi wa sweta,mfuko wa shati langu, na vitabu vyangu, niliviona huko

Niliambiwa nikirudi kwetu nyumbani nitaaga dunia na hiyo ndio ajenda kubwa ya mama wangu wa kambo, nataka kumtobolea baba yangu kuwa sababu kuu ya kutorudi nyumbani ni kwa ajili ya mama wa kambo ambaye aliniroga nisiwahi rudi nyumbani."

Ushauri wako kwa jamaa huyu ni upi?