'Sijifungui watoto mapacha,' Mkewe Khaligraph Jones Georgina azungumza

Muhtasari

•Sibebi mapacha mimba yangu ndio kubwa

•Kulingana na picha mtoto ni mmoja tu 

Khaligraph na mkewe
Image: Hiasani

Mkewe 'rappa' Khaligraph Jones Georgina Muteti amefichua kuwa hatarajii mapacha hii ni baada ya kutangaza kuwa ni mjamzito.

Uvumi umekuwa ukienea kuwa anatarajia mapacha baada ya kuona vile mimba yake imekuwa kubwa kuliko kawaida.

Huku akikana uvumi huo Muteti alisema kuwa hatarajii mapacha kuambatana na ripoti ya daktari lakini ni vile tu mimba yake kubwa.

Khaligraph na mkewe Georgina
Image: Hisani
 
 

Huku akifanya utani Muteti alisema kuwa babake mtoto wake ni jamaa mwenye miraba minne na itakuaje atarajiye mtoto mdogo.

"Tafadhalini sitarajii mapacha, ninaweza kuthibitisha hayo kupitia kwa ripoti ya daktari au ukipenda'Ultra Sound' nilipata ujauzito wangu ni mkubwa.

Mlidhani kuwa nitaenda kuwa na tumbo ndogo kama mpira wa tenisi." Alisema Georgina.

Usemi wake unajiri siku chache baada Georgina na mumewe Khaligraph kutangaza habari njema kupitia mitandao ya kijamii.

(Mhariri Davis Ojiambo)