Mungu alikutuma maishani mwangu kunipa kitu ya kupigania-Vera Sidika amwandikia mwanawe ujumbe

Muhtasari
  • Vera Sidika amwandikia mwanawe ujumbe
  • Vera anatarajia mtoto wake wa kwanza na msanii wa Kenya Brown Mauzo
  • Katika mitandao ya kijamii Vera alitangaza habari za ujauzito wake wiki zilizopita baada ya kuificha kwa miezi 5
Vera Sidika
Vera Sidika
Image: Instagram

Siku moja baada ya kufichua  jinsia ya mtoto wake ambaye hajazaliwa, mwanasosholaiti Vera Sidika amemwandikia barua.

Katika barua fupi lakini tamu, mama mtarajiwa amemsifu binti yake akisema kuwa yeye ni ishara ya matumaini.

Vera anatarajia mtoto wake wa kwanza na msanii wa Kenya Brown Mauzo.

Katika mitandao ya kijamii Vera alitangaza habari za ujauzito wake wiki zilizopita baada ya kuificha kwa miezi 5.

Kulingana na Vera, alificha habari hiyo kwani alijua watu hawatamuamini kamwe.

"Barua kwa Binti yangu ambaye hajazaliwa 📃🖊 Ninaamini kwamba Mungu alikutuma maishani mwangu kunipa kitu cha kupigania, kunionyesha kuna upendo katika ulimwengu huu,

kunipa tumaini na kuniletea furaha, uthibitisho wote kwa Mungu ninaohitaji uko ndani yako. "Daima utakuwa muujiza ambao hufanya maisha yangu kuwa kamili," Aliandika Vera.