"Dalili pekee nimepata ni kukosa hedhi na tumbo kubwa tu!" Vera Sidika azungumzia safari yake laini ya ujauzito

Muhtasari

•Mama huyo mtarajiwa amesema kwamba kando na dalili za kawaida kama kukosa hedhi na kunenepa kwa tumbo amepatwa na kiungulia mara moja na kuumwa na kiuno kwa siku mbili tu.

•Mpenzi huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo amedai kwamba hawezi juta kubeba ujauzito tena  mwaka ujao kwani  kwake imekuwa raha tupu.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti mashuhuri nchini Vera Sidika ameridhishwa na safari yake ya ujauzito huku akieleza kuwa haijakuwa ngumu kama alivyokuwa alivyokuwa amafahamishwa hapo awali.

Kuputia ukurasa wake wa Instagram, mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 31 amedai kwamba safari yake ya ujauzito imekuwa laini na hajashuhudia dalili nyingi.

Mama huyo mtarajiwa amesema kwamba kando na dalili za kawaida kama kukosa hedhi na kunenepa kwa tumbo amepatwa na kiungulia mara moja na kuumwa na kiuno kwa siku mbili tu.

"Nilipata kiungulia mara moja tu.Ilikuwa mbaya lakini ilikuwa kwa siku moja tu na ikaisha. Nilihisi uchungu kwenye kiuno kwa siku mbili pekee na nadhani ni kwa sababu tumbo yangu ilikuwa inanyooka na mtoto alikuwa anasonga juu  chini. Haijanitendekea tena" Vera alisema.

Mpenzi huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo amedai kwamba hawezi juta kubeba ujauzito tena  mwaka ujao kwani  kwake imekuwa raha tupu.

Kulingana na Vera, sio lazima mwanamke mjamzito ashuhudie dalili nyingi kama vile kunenepa kwa kitovu, kupatwa na ugonjwa wa asubuhi, kufura kwa miguu na kulegea kwa mwili. Amedai kwamba kuna baadhi ya wanawake ambao hawashuhudii dalili zozote.

Mwanasoshalaiti huyo ambaye amebakisha wiki chache tu ajifungue amedai kwamba bado anaendelea na kazi zake bila tatizo.

"Miezi nane na nusu na imekuwa safari nyororo. Kusema kweli naweza fanya hivi tena mwaka ujao. Ni raha sana. Nafurahia" Vera alisema.

Vera anatarajia kujifungua mtoto wa kike hivi karibuni.