"Hapa hakuna mahusiano ni kazi tu!" Willy Paul amsajili binti ya staa wa Mugithi Mike Rua katika lebo yake ya Saldido

Muhtasari

•Amesema Saldido International Ent ilimchagua Queen P kwa kuwa alistahili nafasi hiyo huku akimtahadharisha awe makini na watu anaojihusisha nao.

• Willy Paul amefichua kwamba Queen P ni binti ya mwanamuziki wa 'Mugithi' anayeshabikiwa sana nchini Mike Rua.

•Takriban miezi miwili iliyopita Miss P alidai kwamba aligura Saldido kwa kuwa Willy Paul alikuwa anamnyanyasa kingono.

Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Miezi michache tu baada ya msanii wa kwanza kusajiliwa katika lebo ya Saldido International Entertainment, Miss P kuondoka, Willy Paul amemsajili msanii mwingine wa kike.

Siku ya Alhamsi Willy Paul alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kumtambulisha Queen P kama msanii mpya aliyejiunga na lebo yake.

Mwanamuziki huyo aliyezingirwa na drama nyingi katika taaluma yake ya usanii alisema Saldido International Ent ilimchagua Queen P kwa kuwa alistahili nafasi hiyo huku akimtahadharisha awe makini na watu anaojihusisha nao.

"Siku zote ni muhimu kuweka heshima mbele na tamaa nyuma. Kwani ni vigumu sana kwenda mbali bila heshima.. Watu hawapendi kuona wengine wakiendelea kwa hivo kuwa makini sana na unae mpa sikio.. Hata hivyo, nisaidie kumkaribisha msanii mpya wa kike wa @saldido_international. @queenp254 tumekuchagua kwa sababu unastahili nafasi hiyo. Mungu akuongoze katika safari hii.. kuwa makini sana unayejihusisha nae hasa hawa wachekeshaji.. wana vichekesho vingi sana 😆 🤣 😂 Karibu nyumbani.. @saldido_international hits only. Siwezi kusubiri kwa ulimwengu kusikia una nini" Willy Paul aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Akiendelea kutoa maelezo zaidi kuhusu msanii wake mpya, Willy Paul alifichua kwamba Queen P ni binti ya mwanamuziki wa 'Mugithi' anayeshabikiwa sana nchini Mike Rua.

Willy Paul ambaye kwa sasa ana kesi kortini kuhusiana na madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya msanii wake wa zamani Miss P pia amewahakikishia mashabiki kuwa hakutakuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi kati yake na Queen P.

"Kwa wale ambao hamna habari, tumemsajili # MIKERUA BINTI. ndio @queenp254 ni binti Halisi wa Mike Rua.. mwanamke wa Kikuyu mwenye kipaji kikubwa. Sasa twende kumfuata. Yuko tayari kuacha muziki. Nahapa hakuna uhusiano ni kazi tu. @saldido_kimataifa kwa ulimwengu. Letigooooo! Atakuwa na channel yake pindi baada ya miradi yake ya muziki kuwa tayari. huyu ni thitima!" Willy Paul.

Takriban miezi miwili iliyopita Miss P alidai kwamba aligura Saldido kwa kuwa Willy Paul alikuwa anamnyanyasa kingono.