Unastahili kila la kheri,'Rue Baby ammiminia mama yake sifa baada ya kuhitimu chuo kikuu

Muhtasari
  • Rue Baby ammiminia mama yake sifa baada ya kuhitimu chuo kikuu
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamitindo Dion Aggry Okello almaarufu Rue Baby kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemlimbikizia sifa mamake Akothee, siku chache baada ya kuhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Strathmore na kupata digrii ya Uhusiano wa Kimataifa.

Katika chapisho, Rue mwenye shukrani alimmiminia mamake sifa nyingi, akimtaja kama mama asiye na mwenzi ambaye amepigana vita vingi ili kuhakikisha watoto wake wanaishi maisha mazuri.

"Siku hii itakuwa ya kukumbukwa kwangu milele mpenzi wangu @akotheekenya. Kama mama pekee ambaye umeweza kulea watoto wake vizuri katika kizazi hiki unastahili kila la kheri mama.. najivunia kukufanya ujivunie.

Hongera kwa shahada yako ya pili mpenzi wangu. Asante kwa nafasi ya kusoma na kumaliza vizuri. Nakupenda @akotheekenya hongera 🥰🥰🥰🥰,” aliandika Rue Baby.

Baada ya Akothee kuona ujumbe wake Rue alimhakikishia na kumwambia kwamba anampenda zaidi.