'Sitaki upuzi,'Eric Omondi amfokea msanii Bien kwa mara nyingine

Muhtasari
  • Eric Omondi amfokea msanii Bien kwa mara nyingine
Image: INSTAGRAM// ERIC OMONDI

Mchekeshaji na mtunzi wa maudhui Eric Omondi amekuwa akisisitiza mpango wa asilimia sabini na tano wa kucheza muziki wa Kenya.

Amemshambulia tena msanii wa bendi ya Sauti Sol Bien kwa kutounga mkono mpango wake.

Wasanii hao wawili wamekuwa wakizozana kuhusu Bien kukataa kuwa sehemu ya kampeni.

Katika chapisho, Eric alishutumu kuwa na ubinafsi na umaarufu na kukosa kuungwa mkono na wasanii wengine.

Eric ameanzisha kampeni kadhaa ili kuunga mkono muziki wa nchini. Walakini, alikuwa na ujumbe kwa Bien.

"Sijui kama huyu mtu akinyoa Nywele ananyoanga mpaka Akili. Ninapojiandaa KUZINDUA awamu ya PILI na YA MWISHO ya #Cheza75%Mitaa Hakika Ninatatizika Kumuelewa Bien Kiukweli.

Ninashindwa Kuelewa kwanini atakuwa kinyume na SABABU NJEMA kama hii. Bien ni kiongozi wa Sekta na ningemtarajia kwa kawaida kuunga mkono Sababu

Kama nilivyosema awali Bien ni yule Mwanafunzi anataka kupita mitihani Pekee yake, anacheza mpira nanyinyi anaenda funky na nyinyi lakini anasoma usiku

Lakini mimi sitabembeleza Mwanaume Nikianza Awamu ya Pili ya Kampeni sitaki UPUZI na sitavumilia UPUUZI kutoka kwake, BINAFSI NITAMSHUGHULIKIA na hatakupenda. Wakati unakuja ambapo TAIFA zima ni muhimu zaidi kuliko NGUO mmoja mwenye Upara," Aliandika Eric.