'Comrades Triplets' wamemjibu Mwanahabari Amina Abdi

Muhtasari

•Amina alitoa maoni yake kuhusu video  iliyochapishwa na mwimbaji Daddy Owen akielezea kuchukizwa kwake na baadhi za utani  akisema vicheshi hivyo si vya kuchekesha. 

•Watani hao walitarajia kwamba umarufu waliopata kabla ya uigizaji yao kwenye mitandao ya kijamii ungefanya wengi kuitazama baadhi ya kazi yao kule mtandaoni. 

 

COMRADE TRIPLETS
COMRADE TRIPLETS
Image: INSTAGRAM

Cate, Eve, na Mary almaarufu 'Comrades triplets' wamemjibu Mwanahabari Amina Abdi baada ya maoni yake yasiyo sawa kuhusu utani yao dhidi ya watu wasiowafahamu

Watatu hao wamekuwa wakifanya utani kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya video zikisambaa, na huku baadhi ya watu wakistaajabu, wengine kama Amina hawajafurahishwa sana.

Amina alitoa maoni yake  kuptia instagram yake kuhusu video  iliyochapishwa na mwimbaji Daddy Owen akielezea kuchukizwa kwake na baadhi za utani  akisema vicheshi hivyo si vya kuchekesha. 

''Mimi sioni kama kuna kitu cha kufurahia katika utani au ucheshi wanaoifanya, inafaa mtu akuwe  makini sana wakati anafanya ucheshi,unayemfanyia ucheshi anawezakuumia'' Amina alisema.

Katika mahojiano kwenye Youtube, mmoja wa watani hao alisema 'wanashambuliwa' tu kwa kwasababu ya kufaulu katika utani wao.

"Amina aache wivu, amsaidie mtoto wa kike," Mary alisema.

Watatu hao walipata umarufu tangu walipohojiwa na Jalas, ambapo walidai kuwa walikuwa wakitoka na mwanaume mmoja baada ya kumpenda kwa nyakati tofauti.

Siku chache baadaye, ilibainika kuwa watatu hao walifanikiwa kuwadanganya mashabiki wao katika kujenga jina yao.

Hili lilikuwa mojawapo ya matukio mengi ya kusisimua ambayo watu hujihusisha nayo ili kuvutia mashabiki wao kabla ya kuanza uigizaji  yao.

Watani hao walitarajia kwamba umarufu waliopata kabla ya uigizaji yao kwenye mitandao ya kijamii ungefanya wengi kuitazama baadhi ya kazi yao kule mtandaoni.