Hamisa Mobeto afuta jina la Diamond kwa mwanawe

Hata hivyo, miaka kadhaa baadaye, ripoti ziliibuka kuwa Diamond alikataa kumtambua Dylan kama mwanawe.

Muhtasari
  • Uamuzi wa kubadilisha jina la Dylan umechochea uvumi kuhusu hali ya uhusiano wa Mobetto na Diamond na mzozo wa baba unaoendelea.
Diamond na Hamisa
Diamond na Hamisa
Image: Instageam

Ikiwa wewe ni mtumiaji mahiri wa mitandao ya kijamii na unamfuata mwigizaji na mwanamitindo wa Tanzania Hamisa Mobetto, huenda umeona mabadiliko ya hivi majuzi ya majina ya watoto wake kwenye mitandao yao ya kijamii.

Mabadiliko haya yamezua maswali miongoni mwa mashabiki kuhusu sababu za marekebisho hayo.

Mobetto, ambaye ni mama wa watoto wawili, ana mtoto wa kiume na wa kike na wanaume wawili tofauti. Inaaminika kuwa alimzaa mtoto wake Dylan na supastaa wa Tanzania Diamond Platnumz wakati bado yuko kwenye uhusiano na Zari Hassan.

Ujauzito wa Mobetto ulisababisha kukiri kwa umma juu ya uhusiano wao.

Wakati huo Diamond alimchukulia Mobetto kuwa ndiye mwanamke mwingine, lakini alipopata ujauzito, ukweli ulidhihirika hasa baada ya kumuweka hadharani Diamond kuwa baba wa mtoto wake.

Hata hivyo, miaka kadhaa baadaye, ripoti ziliibuka kuwa Diamond alikataa kumtambua Dylan  kama mwanawe.

Katika tukio la hivi majuzi, Mobetto aliamua kubadilisha jina la mwanawe kuwa Dylan Mobetto, na kumtenga na jina la ukoo la Diamond.

Uamuzi wake ulikuja muda mfupi baada ya Diamond kukataa mara kwa mara kumtambua Dylan kama mtoto wake.

Hata hivyo, Mobetto aliamua kuhifadhi jina la bintiye, Fantasy Francis, ili kudumisha uhusiano wake na babake, Mojito Francis.

Uamuzi wa kubadilisha jina la Dylan umechochea uvumi kuhusu hali ya uhusiano wa Mobetto na Diamond na mzozo wa baba unaoendelea.

Mashabiki wengi wameuliza nia ya kubadili jina na inamaanisha nini kwa siku zijazo.

Mwanablogu Mtanzania Millard Ayo alifanya mahojiano kwa njia ya simu na mamake Hamisa Mobetto ili kupata ufahamu kuhusu uamuzi wa Mobetto na sababu zake za msingi.

Akijibu maswali kuhusu uamuzi wa bintiye, mama yake Hamisa alieleza kuwa wakati wao mitandao ya kijamii kama Instagram haikuenea, na kupendekeza kuwa mabadiliko hayo yanaweza kuwa ya kawaida sasa.

"Hilo swali anatakiwa ajibu Hamisa...Sisi wakati tunawazaa hakukuwa na Insta jamani lakini nathani haya ni mambo ya kawaida tu jamani.... Atawajibu kwa ufasaha kabisa. Wazungu wanasema 'Time will tell' " Mama Mobetto alisema.

Alisisitiza kuwa ataendelea kumuunga mkono na kumtetea binti yake bila kujali uvumi wa umma.