Boniface Mwangi afichua namba iliyokuwa inamtishia msanii Juliani

Muhtasari
  • Boniface Mwangi afichua namba iliyokuwa inamtishia msanii Juliani
Lilian Ng'ang'a na Juliani
Image: Boniface Mwangi/Twitter

Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Boniface Mwangi ameanika nambari ya simu inayotumiwa na watu wasiojulikana, na kutishia kumuua Mwanamuziki Julius Owino maarufu Juliani juu ya uhusiano wa kimapenzi na LIlian Ng'ang'a.

Mwangi alisema kuwa tayari Juliani ameandika taarifa katika kituo cha Polisi cha Kileleshwa juu ya vitisho hivyo.

Kulingana na Mwangi, Juliani ametakiwa kuacha kupakia picha alizopiga na Lillian la sivyo watamuua.

“Rafiki yangu mzuri sana @JulianiKenya alitishiwa jana. Kuna mtu alimpigia simu na kutuma ujumbe mfupi akitumia 0773912088

Alimwambia aache kuweka picha zilizopigwa na rafiki yake @LillyanneNganga, na ikiwa ataendelea, watamuua. Ameandika taarifa katika Kituo cha Polisi cha Kileleshwa ”alishiriki Boniface Mwangi kupitia mtandao wake wa Twitter.

Kauli yake inakuja masaa kadhaa baada ya Juliani pia kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter, akisema kwamba amekuwa akipokea vitisho juu ya madai ya kuiba mke wa Gavana Alfred Mutua.